Katibu wa Mwanza Pastors Free Fellowship Mchungaji Aoron Rubango akitoa maelekezo juu ratiba za maombi kama anavyoonekana pichani.
Muda wa kuabudu nao ulifika na hapa uwanja mzima ulizizima kwa sifa na uabudisho mkuu ambao uliongozwa na roho mtakatifu.
Shuka bwana kwa uweza na Munguu, wimbo ukiendeleaaaaaa
Mpiga kinanda nae hakuwa nyuma kupapasa kinanda cha muziki laini hadi watu wakazama ndaniiiiiii.
Hivi ni kwaya ya Bonde la Baraka kutoka kanisa la EAGT Bonde la Baraka chini yake Mchungaji Aron Rubango wakiwajibika kwa stageeeeee.
Watu wakiendelea kufuatilia kila tukio linaoendelea katika uwanja wa Nyamagana.
Sifa inogileeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, kila mmoja kujiachia kivyakeeeee.
Fabian Fanuel, Mwanza.
Mwanza Pastors Free Fellowship wamekutana mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Nyamagana kwa kusudi kubwa la kuliombea Taifa la Tanzania na kanisa ili liwe na amani ya kutosha.
Maombi hayo yalioanza saa nne za asubuhi, wakirsto kutoka madehebu mbalimbali walikutana kwa ajili ya:
1. Kuliombea Taifa la Tanzania na viongozi wake toka ngazi za juu hadi ngazi za chini.
2. Kuombea amani, umoja na mshikamano katika Taifa la Tanzania.
3. Kuombea Kanisa na kazi ya Mungu duniani.
4. Kuombea Viongozi wa madhehebu yote katika kuleta amani upendo na umoja katikati ya kazi ya Mungu.
5. Kuombea Bunge na upatikanaji wa katiba.
6. Uchaguzi wa 2015.
Akifungua maombi hayo,Katibu wa Chama cha Mwanza Pastors Free Fellowship Mch. Aoron Rubango alisema kuwa huu ni Mwanzo mzuri katika kutekeleza mikakati waliojiwekea katika chama chao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja huu Mch. David Emmanuel amewaasa Watanzania wote kuwa kitu kimoja katika kuiombea kazi ya Mungu na Taifa kwa ujumla.
Watu kutoka madhehebu mbalimbali jijini Mwanza walijitokeza kushiriki maombi hayo ikiwa ni pamoja na wachungaji na maaskofu kutoka madhehebu mbalimbali.
Tupe maoni yako