HISTORIA YA KANISA KWA
UFUPI
Kanisa la K.k.k.t Yerusalemu mabatini
Mwanza lilianza mwaka 1960 likiwa chini ya Mwinjilisti Ella Pyuza ambaye kwa
sasa ni marehemu,kwa wakati huo walikuwa wakiabudia katika majengo ya Laini
polisi Mabatini Mwanza.Baada ya muda kupita walihama pale walipokuwa wakiabudia
na kuelekea katika Shule ya Msingi ya Pamba Primaly school iliyopo Mabatini
Mwanza hapo ndio wakawa wakiabudia wakiwa chini ya Mwinjilisti Mwakalasia na
baada ya muda kupita walipata kiwanja kilichopo maeneo ya Mabatini Mwanza na
wakaanza ujenzi wa kanisa huku wakishirikiana na waumini pamoja na mafundi na
mwaka 1996 walianza kusali katika kanisa walilolijenga na kwa wakati huo
ulikuwa ni Mtaa wa Yerusalemu Mabatini ukiwa chini ya Mwinjilisti Pendaeli
Ulio, na baada ya muda kupita wakapata nafasi yakuwa Ushalika wa Yerusalemu
Mabatini huku ukiwa chini ya Mwinjilisti William Msokwa.
MAFANIKIO YA KANISA KWA UFUPI
Kanisa
la Yerusalemu mabatini Mwanza K.k.k.t limeweza kufanikiwa kufungua kanisa
lingine ambalo lipo mtaa wa Mahina Mwanza ambapo kanisa ilo linatambulika
kwajina la Mtaa wa Bethania Mahina K.k.k.t,pia Ushalika wa Yerusalemu Mabatini
umefanikiwa kuweka vigae ndani yakanisa,pamoja na mengine mengi.
HISTORIA
YA KWAYA YA NEEMA/KUANZA KWAKE.
Kwaya ya Neema ilianzishwa mwaka 1997
ikiwa chini ya Mwenyekiti Aliko Ibrahim, ikiwa na waimbaji kumi na tatu (13)
chini ya mwalimu Jacobo Mwaikibaya, wakati huo wakiimba kwa kutumia vyombo vya
asili kama vile Ngoma, Filimbi, Chupa za Soda n.k, Neema kwaya ilianza na
waimbaji kumi na tatu (13) ambao kwa majina yao ni; Boniphace Mwandunga, Jacobo
Mwaikibaya, Ibrahim Aliko, Emmanuel Nkombe, Samwel Marick, stella Fredy
Mwasilembo, scolastika Fredy Mwasilembo, Nuru Makea Mwambemba, Dorah Makea
Mwambemba, Aliko Wanki, Richard Robert, Esther Robert, Mr’s Tito, Pia kwa
wakati huo kwaya ilikuwa na mlezi mmoja ambaye ni Mzee Mwambemba ambaye kwa
sasa ni Marehemu.
MABADILIKO
YA UONGOZI.
Kwaya ya Neema tuliamua kufanya uchaguzi
wa viongozi wa kwaya mnamo mwaka 2004, kwa kuanza na ngazi ya Mwenyekiti
tulimchagua ndugu Jacobo Mwaikibaya kama Mwenyekiti mkuu wa kwaya na Msaidizi
wake alikuwa ni Andrea Andrew, huku katibu alikuwa ni ndugu Mr Francis na
katibu msaidizi alikuwa ni Edward Somi. Pia mnamo mwaka 2007 kwaya ilifanya
uchaguzi mwingine wa viongozi baada ya kuwa uongozi uliopita muda wake kuwa
umeisha na wengine kuhama, ambapo mwenyekiti tulimchagua ndugu Colnel Siyola,
msaidizi wake akiwa Loyce Andrea na
katibu tulimchagua ndugu Edward Somi na msaidiizi wake akiwa ni Frola Daudi
ambaye pia ndiye Mwalimu wa kikundi, pia kwaya ilimchagua ndugu Nickson Petro
kuwa mtunza hazina wa kwaya. Kwaya ya Neema iliamua pia kufanya uchaguzi wa
walezi ambao kwa majina yao ni; Loyce Maulilo, Samwel Marick, Blanka Ngoi na
Anneth Limo, pia kwaya ilimchagua M’rs Eliyawinga Mungule kuwa Mshauri wa
kwaya.
MAFANIKIO
Kwaya ya Neema tulifanikiwa kununua
vyombo vya muziki vya kisasa kwa kuchangishana wanakwaya na zingine kuchangiwa
na kanisa na tukaweza kununua, Kinanda PSR 1100, Speaker mid mbili (2), na
Stendi za Speaker mbili (2).
Mnamo tarehe 17/11/2009 kwaya ya Neema
tulifanikiwa kurekodi Albam ya kwanza ambayo ni Audio iitwayo MOTO WA JEHANAM
tuliyoirekodia katika Studio ya Habari Maalum. Na ilipofika mwaka 2010 kwaya ya
Neema tulizindua Albam hiyo iliyofahamika kwa jina la MOTO WA JEHANAM Katika
viwanja vya kanisa la K.K.K.T Mabatini Mwanza.
Pia ilipofika mwaka 2011 kwaya ya Neema
tulirekodi Audio ya pili na kutoa mkanda wa Video katika studio ya One Love
Studio. Na mnamo mwaka 2015 kwaya ya Neema tulifanikiwa kuzindua albam hiyo
katika viwanja vya kanisa la K.K.K.T Mabatini Mwanza. Pamoja na mafanikio hayo
yote kwaya ya Neema kwa sasa tuna jumla ya waimbaji ishirini na tano (25)
ambapo waimbaji wa kiume idadi yao ni waimbaji kumi na tano (15) na idadi ya
waimbaji wa kike ni kumi (10).
Na pia tunapenda kuwashukuru wale wote ambao
walikuwa wakishirikiana nasi na bado wanaendelea kushirikiana nasi kwa kutupa
michango yao ili kuhakikisha kikundi hiki kinapiga hatua, tunawashukuru
viongozi na waumini wote wa Yerusalem Mabatini pamoja na watu binafsi bila
kusahau Media zote ambazo zimekuwa zikitupa ushirikiano kwa kupiga nyimbo zetu
hasa Redio kwa Neema fm bila kumsahau Fabian Fanuel kwa ushirikiano ambao anaendelea
kuuonesha. Hivyo tunasema Mungu awabariki sana.
CHANGAMOTO
Siku zote palipo na mafanikio huwa
hapakosi changamoto, kwaya ya Neema tunazo changamoto nyingi sana katika huduma
hii ambazo ni pamoja na;
(a) Ukosefu wa vyombo vya muziki hasa
baada ya kuunguliwa na vyombo vyetu vyote (b) Ukosefu wa usafiri wa uhakika
pindi kwaya inapokuwa na safari ya kupeleka injili sehemu mbalimbali (c)
Ukosefu wa wataalam wa muziki, hivyo inakuwa inatulazimu kutoa pesa kwaajili ya
kupigiwa muziki (d) Ukosefu wa walimu ambao ni watunzi wazuri wa nyimbo (e)
Kwaya inaukosefu wa miradi na hivyo kutulazimu kuchangishana pesa wenyewe kwa
wenyewe ili tuweze kupata kile tunachohitaji.
MALENGO
YA KWAYA
Kwaya ya Neema tuna malengo mbalimbali
ambayo ni kama ifuatavyo; (a) Kwaya ya Neema tuna malengo ya kununua vyombo vya
muziki vya kisasa (b) Pia tunayo malengo ya kuanzisha miradi midogo midogo (c)
Tuna malengo ya kurekodi audio na Video.
MIKAKATI
YA KWAYA YA NEEMA/MALENGO TARAJIWA
Kwaya
ya Neema tunamikakati mingi sana ambayo Mungu akitupa Neema tungependa
kuyakamilisha,mikakati hiyo nikama ifuatavyo,(a)Mungu akitupa neema tunatarajia
kununua kiwanja cha kujenga maduka 5 yakukodisha, pamoja na shule ya awali ya
chekechea.(b)Pia tunatarajia kununua costa 2 kwaajili ya biashara ili kwaya
iweze kunufaika katika suala zima la kujikimu kifedha na kiuchumi.Yote haya
tutayakamilisha pale ambapo tutapata neema ya kupata wafadhili wakutuwezesha
ili yote yaweze kutimia.
MAHITAJI
YETU KAMA KWAYA
Kwaya ya Neema tuna mahitaji mbalimbali
ili tuweze kupiga hatua zaidi na mahitaji yenyewe ni kama ifuatavyo; (a)
Tunahitaji kuwa na kompyuta ili tuweze kutunza kumbukumbu za kwaya kwa ufasaha
zaidi. (b) Tunahitaji kuwa na GARI la usafiri litakalotuwezesha kutoa huduma au
kupeleka Neno la Mungu sehemu mbalimbali kwa urahisi (c) Pia tunahitaji kupata
wafadhiri ambao wataweza kutusaidia katika huduma hii ya uimbaji
WITO
KWA KWAYA
Tukiwa kama kwaya ya Neema tunatoa wito kwa
kwaya zingine kuwa huduma hii ya umbaji ina changamoto nyingi sana, hivyo
ni muhimu kuwa na umoja mzuri pindi
tunapokuwa na wanakwaya wetu. Pia tunatakiwa kuwa wavumilivu kwani kuna kukata
tama na mwisho ni kikundi kuvurugika, ni muhimu sana kusimama katika maombi na
kumsihi Mungu aweze kutuinua katika huduma hii, na ni vizuri tuwe na nidhamu
kwa viongozi wetu wa makanisa na viongozi wa kwaya na tuweze kushirikiana na
jamii vizuri ili waweze kumjua Mungu kwa kupitia nyimbo zetu.
Kuwapata unaweza kuwasiliana nao kwa
mawasiliano yao kama ifuatavyo:
Po box Number 11592.
Phone
Number 0756-831375/0625-812573 Mwenyekiti.
0767-154418/0624-129297
Katibu.
Tupe maoni yako