Na Magreth Kinabo, MAELEZO
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid amesema zaidi ya 35,000 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa wa saratani.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid amesema zaidi ya 35,000 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa wa saratani.
Kauli hiyo imetolewa leo na waziri huyo wakati akitoa tamko kuhusu Siku ya Saratani Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Februari 4 kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.
Aidha Dk. Rashid katika kuaadhimisha siku kutoa upimaji Februari 4 na 5, mwaka huu bure, hivyo aliitaka jamii kujitokeza mapema ili kupima ugonjwa huo. Alisema huduma za ugonjwa huo ni haki ya kila mtu na matibabu yake ni bure.
“Hapa Tanzania tatizo la Saratani limekuwa likiongezeka mwaka hadi mwaka. Kila mwaka jumla ya wagonjwa wapya wa Saratani 44,000 hugundulika na zaidi ya 35,000 hufariki kutokana na ugonjwa huu,” alisema Dk. Rashid.
Aliongeza kuwa takwimu za Taasisi ya Saratani Ocean Road, zinaonyesha kwamba kila mwaka inapokea wagonjwa wapya wa Saratani 5,000. Wagonjwa hao wanakuja wakati Saratani ikiwa katika kiwango cha juu - yaani hatua ya 3 na 4; na inasababisha uponaji wake kuwa mgumu.
Kauli mbiu ya maahimisho ya siku ya Saratani kwa mwaka huu ni “Kupunguza unyanyapaa na kuondoa dhana potofu kuhusu Saratani”.
Aidha Dk. Rashid alisema saratani inayoongoza hapa nchini kwa wanaume ni Saratani ya Kaposi na Saratani ya Tezi Dume imekuwa ikiongezeka , na wanawake, Saratani ya Shingo ya Kizazi.
Serikali katika kuboresha imeanzisha huduma hizi katika Hospitali ya Bugando, baadae itaanzishwa katika Hospitali za Rufaa za KCMC na Mbeya.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Twalib Ngoma alisema utafiti uliofanywa unaonesha kuwa tumbaku huchangia wagonjwa wa saratani kwa asilimia 40 .
Tupe maoni yako