Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, imesema taarifa ya miradi ya maendeleo ya Jiji la Mwanza ni mbaya kuliko za majiji mengine yote. Hivyo imetoa siku 90 kwa halmashauri hiyo kuandaa taarifa mpya na sahihi.
Kamati hiyo ipo Mwanza na jana ilikuwa ikipokea taarifa ya utekelezaji miradi.
Agizo hilo limekuja baada taarifa ya
awali kukataliwa na kamati hiyo iliyokuwa ikifuatilia taarifa ya miradi
hiyo takriban wiki moja iliyopita, bila ya kupata majibu sahihi ya
upungufu kwenye miradi kama ilivyosomwa na Mkurugenzi wake, Halipha
Hida.
Akizungumza na watendaji hao, mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Hamisi Kigwangala alisema wameshindwa kuwawajibisha watumishi hao ipasavyo, kutokana na kuwa mara ya kwanza kwao kufanya kazi halmashauri hiyo ambayo haijawahi kufanyiwa ukaguzi tangu kuundwa kwake.
"Tangu tuanze kufanya kazi kupitia kamati yetu hii na majiji yote, hatujawahi kuona uandaaji taarifa mbaya kama ya Jiji la Mwanza," alisema Dk Kigwangala.
Dk Kigwangala alisema kamati haijapendezwa na baadhi ya miradi ya ujenzi kituo cha afya ya mama na mtoto, stoo ya dawa na ofisi ya mganga mkuu inayojengwa.

Tupe maoni yako