banner

.

.

Monday, 10 February 2014

USIYOYAJUA KUMHUSU BEN PAUL

Benard Michael Paul Mnyang’anga au unaweza kumuita ben pol alizaliwa september 8, mwaka 1989. Kwasasa ben pol ndiyo mfalme wa muziki wa Rnb hapa Tanzania na Vibe tulipata nafasi ya kukaa na king huyu na kupiga story mbili tatu kuhusu muziki anayofanya alipotokea na anapoelekea.
 
Ben pol alianza kufanya muziki zamani sana lakini tofauti na sasa anavyofanya muziki kama kazi zamani ilikua ni kama burudani yake na washkaji zake. “Tangu mwaka 2007 nilikuwa nafanya muziki, ili bado nilikuwa nafanya kama kujifurahisha,nilikuwa nawaimbia washkaji shule, then baadae nikaingia THT , nimekaa THT kwa miezi6, baadae nikarudi shule, niliingia pale azania kufanya form5 na 6 “ alisema ben pol.
Ben-Pol-2

Safari yake ya muziki haikuishia hapo, kama wanamuziki wengi watafutaji ben pol aliendelea kutafuta channel ya kutokea katika muziki. “ Kabla sijatoka kimuziki nimeshawahi kushiriki BSS(Bongo Star Search) ila bahati mbaya sikupata nafasi ya kutoka,ila kiukweli nilijifunza mengi sana kwa kushiriki bongo star seach, kwasababu nilivofika pale, nikakuta watu wanajiandaa kwelikweli, wengine wamekuja na magitaa, wengine ndo wanapractice palepale yaani nikaamini kweli watu wakitaka kufanya kitu wanajipanga. “

Tupe maoni yako