· Ni katika kinyang’anyiro cha kuwania
kombe la dunia.
· Macho na masikio ya wapenzi wa soka
duniani kuelekezwa Brazil mwaka huu.
Kamakawaida wewe shabiki mkubwa wa kisima cha burudani
tunaendelea kufahamishana habari kemkem za kiburudani zinazoendelea katika ulimwengu wa
burudani kama tulivyoanza awali kukufahamisha kukamilika kwa baadhi ya viwanja
vitakavyotumika katika kipute kijacho cha kombe la dunia kwa mwaka huu wa 2014
nchini Brazil sasa tunakufahamisha vikosi vya timu shiriki na nyota wake na leo
hii tunaanzia na wawakilishi toka barani afrika ambapo bara hilo linawakilishwa
na timu tano.
Cameroon simba
wasioshindika simba wanyika ni miongoni
mwa timu zitakazo iwakilisha Africa katika michuano hiyo huko brazil
ikiongozwa na kocha Volker Finke na
itakuwa ikimtegemea zaidi nyota wake Samwel etoo Phil anayekipiga kwenye club
ya Chelsea ya England kama chachu ya ushindi pamoja na wachezaji wengine kama
akina Steven mbia anayecheza soka la kulipwa kwenye club ya Olympic maseyii ya
nchini ufaransa,joel matip anayekipiga na shalke 04 ya ujerumani na wengineo
wengi.
Timu ya Taifa ya Cameroon
Ghana maarufu kama black stars brazil ya Africa mashabiki wa
soka barani Africa waliweza kuthubutu kuiita hivyo kutokana na soka ya kutandaza pasi za uhakika
itaongozwa na kocha James Kwesi Appiah na watakuwa na vifaa wao akina Michael essien Asamoa Gyan
Sule muntari na wengineo wao watakuwa kundi G na timu za
ujerumani,ureno pamoja na marekani.
Timu ya Taifa ya Ghana
Ivory coasty hawa ni tembo maarufu wakifahamika hivyo ni
timu nyingine itakayo iwakilisha Africa katika michuano hiyo ya kombe la dunia
kwa mwaka 2014 nchini brazil itakuwa ikinolewa na Sabri lomauchi na ikiwategemea nyota wake
kama Didier drogba Yaya toure nduguye kolo toure itakuwa kundi c pamoja na timu
za Colombia,Ugiriki na japani.
Timu ya Taifa ya Ivory Coast
Algeria maarufu kama mabwea wa jangwani fennec
foxes hawa ni wawakilishi wengine
kutoka kaskazini mwa bara la Africa wakiwa na kocha wao Vahid Halihodzic na watakuwa wakiwategmea
akina majid boughera anayekipiga kweny
club ya lekhwiya,ryad boudebouz anayekipiga katika timu ya bastia
ya nchini ufaransa ambapo watakuwa na upinzani mkali na timu za urusi ubelgiji na jamhuri ya watu wa korea
katika kundi h.
Timu ya Taifa Algeria
Nigeria super eagles wakiwa na kocha mzalendo na aliyepata
mafaniko makubwa na timu hiyo kwa siku za karibuni baada ya kunyakuwa ubingwa
wa Africa Steven keshi wao watakuwa na matumaini makubwa kwani wanajivunia
kikosi kilichosheheni nyota kibao wanaosakata kandanda la kulipwa barani ulaya
kama akina John mikel Obi,Uche, mlinda mlango Vicent Enyeama na wengineo ambao watakuwa nchachu ya ushindi katika
mechi zao za kundi f wakiwa na timu za Argentina,Boznia
and Herzegovina na iran.
Timu ya Taifa ya Nigeria
Tupe maoni yako