banner

.

.

Saturday, 15 February 2014

KAMPUNI YA TIGO TANZANIA YATAMBULISHA HUDUMA TIGO KILIMO KWENYE KONGAMANO YA UWEKEZAJI MWANZA....


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal akizungumza na Mkurugenzi wa Kanda ya Ziwa kutoka Tigo Bw. Ally Maswanya juzi wakati wa Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa unaomalizika leo jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na mmoja wa maafisa wa Tigo makao Makao Makuu Irine Kiwia, mara baada ya kutembelea banda la Tigo na kubainishiwa huduma mbalimbali zilizoingia sokoni ikiwepo huduma ya mtandao wa internet inayojulikana kwa jina la TIGO KILIMO ambayo kwayo mkulima anapata fursa ya kujua bidhaa na pembejeo mbalimbali za kilimo anazo hitaji ikiwemo bei ya manunuzi kwa pembejeo hizo pamoja na maduka, huduma za waghani (maafisa kilimo), masoko na kadhalika. 
Mkurugenzi wa Kanda ya Ziwa kutoka Tigo Bw. Ally Maswanya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kufafanua huduma mbalimbali za TIGO hususani huduma mpya ya TIGO KILIMO wakati wa Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa unaomalizika leo jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa Kanda ya Ziwa kutoka Tigo Bw. Ally Maswanya (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walio shiriki Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa unaomalizika leo jijini Mwanza.

Tupe maoni yako