|
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Msukuma akizungumza na waandishi wa habari hii leo katika ukumbi wa CCM mkoa wa Mwanza. |
WENYEVITI wa CCM mikoa ya
Tanzania bara wametoa tamko la kumkana Mwenyekiti wa Umoja wa Wenyeviti
CCM Taifa Mgana Msindai, na kutishia kumvua madaraka ya Uenyekiti wa
Umoja huo, kwa kuwauza wenyeviti wenzake kwa watu wanaotarajia kugombea
urais kabla ya muda na utaratibu wa Chama kufika.
Hatua hiyo inafuatia tamko lililotolewa kwa niaba ya Wenyeviti wa CCM wa
mikoa ya Tanzania bara Joseph Msukuma (Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita)
leo jijini Mwanza akipinga kauli iliyotolewa hivi karibuni na Msindai
ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, wakati alipoalikwa katika
sherehe ya kuuaga na kuukaribisha mwaka mpya wilayani Monduli, hafla
iliyoandaliwa na Mjumbe wa NEC na mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa
ambapo Msindai katika salamu zake alinukuliwa na vyombo vya habari na
taarifa zake kutoka leo akisema kuwa yeye pamoja na wenyeviti wa CCM wa
mikoa yote nchini wako nyuma ya Lowassa wakimuunga mkono, kauli ambayo
imewaweka katika wakati mgumu wenyeviti wa CCM mikoa mbalimbali hapa
nchini ikihofiwa kuanza kuwagawa wananchi na kutengeneza makundi.
|
Sehemu ya wanahabari, kutoka kulia ni John Maduhu (Mtanzania), Mashaka Bartazar (Majira) na Deus Bugahilwa. |
|
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Msukuma akizungumza na waandishi wa habari hii leo katika ukumbi wa CCM mkoa wa Mwanza. |