banner

.

.

Saturday, 8 February 2014

Waziri wa kigeni wa Kenya azuru Ujerumani



ujerumani_3ff13.jpg
                            Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya, Amina Mohamed

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Kenya, Amina Mohamed, anazuru Berlin, Ujerumani. Jana (06.02.2014) alikutana na viongozi wa makampuni na mashirika ya kibiashara na kusisitiza umuhimu wa uwekezaji Kenya.

Akizungumza kwenye mkutano uliondaliwa na shirika la Ujerumani linaloshughulikia ushirikiano na bara la Afrika, waziri Amina Mohammed alisema Kenya imefungua milango yake kwa Ujerumani kufanya biashara kwa kuwa ndiyo iliyokuwa nchi ya kwanza kuutambua uhuru wa Kenya mnamo mwaka 1963.

 Amedokeza kwamba kampuni ya Ujerumani ya Bosch tayari imefungua ofisi yake jijini Nairobi wiki iliyopoita, ishara kwamba kampuni za Ujerumani zina imani na mazingira ya kibiashara katika taifa hilo.

Tupe maoni yako