banner

.

.

Thursday, 20 February 2014

WATU WANNE WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA LORI LA MAFUTA LILILOPINDUKA NA KUTEKETEA KWA MOTO.


Wananchi waliokuwa safarini katika njia hiyo,wakiangalia Lori hilo baada ya kuteketea kwa moto.
                Mabaki ya Lori hilo baada ya kuteketea kabisa na moto jioni ya jana.
 
              Hivi ndivyo hali ilivyokuwa baada ya Lori hilo kuteketea kwa moto huo.
 
 Mashuhuda wakiwa chini ya Bonde la mlima sekenke,lilipo Lori lililoteketea kwa moto.
 
Lori la mafuta limeanguka na kuteketea kwa moto jioni ya leo katika eneo la milima ya sekenke mkoani Singida na kupelekea watu kadhaa kupoteza maisha hapohapo (idadi yake haijathibitishwa Jeshi la Polisi). Chanzo cha ajali hiyo,bado hakijafahamika mpaka sasa,japo kuna tetesi kuwa gari hilo lilifeli breki wakati likiteremka kwenye milima hiyo.
Shuhuda wa ajali hiyo,aliejitambulisha kwa jina la Bwana Julius Chacha alimueleza Ripota wetu kuwa,Lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia bondeni huku likikianza kushika moto.
Shuhuda huyo aliendelea kusema kuwa,walishindwa kutoa msaada wowote kwa wakati huo kwani moto uliposhika ulikuwa mkubwa sana na hawakuwa na vifaa vya kuokolea.
Mpaka Ripota wetu anaongoka eneo la tukio,hakukuwa na Polisi walikuwa wamefika katika eneo hilo la tukio.
 CHANZO:MTAA KWA MTAA

Tupe maoni yako