banner

.

.

Monday, 10 February 2014

TFF yaahidi kujenga vituo vya soka 169

tff-july5-20131 aee39
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lipo mbioni kujenga vituo 169 vya michezo katika wilaya 169 za Tanzania.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema kuwa licha ya vituo hivyo kufundisha soka pia ni maalumu kwa ajili ya kufundisha vijana juu ya athari za matumizi ya dawa za kulevya.
Hivi karibuni Malinzi alizindua kampeni ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana iitwayo Ishi Huru, ambayo inaratibiwa na Taasisi ya African Inside Out wakati TFF ni washiriki wakuu.
"Katika hili kupitia idara yetu ya ufundi, tupo mbioni kufanya sensa ya vituo vya kukuza na kulea vipaji vya vijana pamoja na vituo vya mpira nchini kote. Utaratibu huu unafanywa kwa kuwekwa vigezo vya kutambuliwa vituo hivyo na TFF itaweka utaratibu wa kusajili na kutoa vyeti vya usajili kwa kituo kitakachokidhi vigezo.
Malinzi alisema kuwa lengo ni kuweka utaratibu nchini wa kusimamia na kuendeleza vituo hivi kitaifa na kwamba ili Tanzania ifundishe mpira unaofanana nchi nzima wanaandaa utaratibu wa kuandaa mitalaa
ya kufundisha mpira.
Alisema mtalaa huo unaandaliwa na idara ya ufundi ya TFF kwa kusaidiana na mtaalamu wa mpira kutoka Uholanzi na kudai kuwa mtalaa huo ukikamilika utakuwa nyezo muhimu ya kufundishia mpira shuleni na kwenye vituo vya kuendeleza soka.
Katika hatua nyingine Malinzi alisema uongozi wake pia umeandaa mpango wa kukutana na wenyeviti wa vyama vya tiba, waamuzi na makocha ili kupanga mikakati ya maendeleo ya kitaaluma.
"Mikakati hii ambayo itajumuishwa katika mpango mama wa maendeleo wa TFF, maandalizi yake yatakamilika ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa." Chanzo: mwananchi

Tupe maoni yako