Misaada
ya hali na mali imeanza kumiminika kwa ajili ya Aida Nakawala (25)
mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye
alijifungua watoto wanne mapacha kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa
kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini
Mbeya.
Msamaria
mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ametuma maboksi mawili yenye
nguo na vitu kadhaa vya watoto, ambavyo vimewasili salama katika ofisi
za Michuzi Media Group (MMG) inayoendesha Globu ya Jamii jijini Dar es
salaam baada ya kusafirishwa bure na Wazee wa Kazi, Serengeti Freight
Forwarders ya huko Uingereza.
Hivi
sasa MMG ikishirikiana na waratibu wa misaada kwa mama huyo, wanaandaa utaratibu wa kumfikishia Mama Aida mizigo yake haraka
iwezekanavyo.
NA MBEYA YETU BLOG |
Tupe maoni yako