banner

.

.

Thursday, 13 February 2014

LUCAS SINKALA MWENDA KUGOMBEA UBUNGE KALENGA KWA TIKETI YA CHADEMA .

c24_86467.jpg
Bw. Lucas Sinkala Mwenda amechaguliwa kuiwakilisha CHADEMA katika nafasi ya kugombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia kura za maoni zilizopigwa na jumla ya wajumbe 407 wa chama hicho katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa St. Dominic katika manispaa ya Iringa, jumla ya kura 407 zilipigwa na hakuna kura iliyoharibika hivyo mwakilishi huyo amepata jumla ya kura 132 na kufanikiwa kuwapiku wagombea wenzake lakini bado hajapitishwa rasmi kwa kuwa anasubiri maamuzi rasmi kutoka katika kamati kuu ya chama hicho yatakayofanyika tarehe 14/2/2014, hivyo wagombea wote 13 wanatakiwa kuwasili kwenye mkutano wa kamati kuu ya chama utakaofanyika tarehe hiyo, Dar es Salaam.
c23_47c65.jpg
c41_7ec05.jpg
Mkurugenzi mwezeshaji wa mafunzo ya chama hicho Bw. Benson Kigaila akitoa maelekezo na utaratibu kwa wajumbe hao wa CHADEMA kuhusu namna ya upigaji kura na umuhimu wake katika maendeleo ya chama hicho na taifa kiujumla.
c47_92e9c.jpg
Mbunge wa viti maalumu, kupitia chama cha CHADEMA mkoani Iringa, Bi. Chiku Abwao akiongea na wajumbe wa Chadema kwenye mkutano huo wa uchaguzi wa Mbunge atayekiwakilisha chama hicho kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo la Kalenga, mkoani Iringa.
c44_ecfc3.jpg

Tupe maoni yako