Wengi
wetu tumekuwa tukisikia kuwa kuna wadudu watamu sana na hupatikana sana
hasa katika msimu wa Mvua, wadudu hao ambao ni Maarufu kwa jina la
Kumbikumbi huanza kujitokeza wakati wa mvua hasa katika vichuguu vyao
vikubwa ambavyo hufaamika kwa kuishi wadudu wengine wanaojulikana kwa
jina la mchwa hawa hugeuka na kuja kuwa kumbikumbi.
Mkoa
wa Mbeya ni moja ya maeneo ambayo kunapatikana kumbikumbi kwa wingi
sana ..Kupitia ukurasa huu wa leo tutapata kujionea
jinsi kumbikumbi hao wanavyopatikana.
Hiki ni kichuguu ambacho kimefunikwa kwa umahili kabisa, ambapo kote hakuna mwanga isipokuwa sehemu moja tuu.
Hili
ni Tundu dogo maalumambapo kumbikumbi hawa hupumbazika na mwanga huu
wakijua kuna mwanga ili watoke na ndipo wanapo kamatwa
Hii
ni ndoo ambayo imetegeshwa katika Tundu dogo ambapo panatoka Mwanga ,
hapa ndipo kumbikumbi hawa wanapotokea na kudumbukia katika ndoo hiyo na
hatimaye kushindwa pa kutokea
Picha
hii inaonesha Jinsi kumbikumbi waliochanganyikana na Mchwa wakiwa
wamedondokea katika Ndoo maalum ambayo hapa ni mtego wa kuwatega
Kumbikumbi hawa.
Anaitwa Bwana Edward ambaye ni mtaalam wa kuandaa vichuguu hivyo, hapa alikuwa akihakikisha kama kweli kuna kumbikumbi hao.
Hii ni aina tofauti ya Kichuguu ambacho kimejitokeza pembezoni mwa shamba.
Huu ni aina nyengine ya mtego wa kumbikumbi hao
Hii ni Njia ambayo kumbikumbi hao wanakuwa wakitokea huku wakifuata mwanga watoke na kujikuta wapo mtegoni.
Juu ni vichuguu ambavyo bado havijatengenezwa , vikiwa vinaandaliwa kwa ajili ya kuwatega kumbikumbi hao.
Mbeya yetu blog
Tupe maoni yako